Hapa chini ni mambo muhimu ya kufahamu kabla hujanunua TV. Tumeandaa muongozo huu kukusaidia kufanya maamuzi sahihi unaponunua TV.
Vitu muhimu unavyotakiwa kufahamu kwenye TV
1: Aina ya kioo (display type)
2: Resolution ya TV (Hii inahusu ubora wa picha kwenye tv)
3: Technology ya TV
4: Size ya TV
Kitu muhimu cha kuzingatia unaponunua TV ni kioo chake. Kuna aina 3 za vioo vya TV ambavyo ni LED, LCD na plasma. LED ni maarufu sana na ina jamii tatu LED, OLED na QLED
Sifa za LED TV
Sifa za QLED TV
Sifa za OLED TV
TV resolution ni namba ya vidoti vidogo vidogo sana (pixels) vinavyotengeneza picha kwenye televisheni yako. Kadri vidoti vikiwa vingi ndivyo picha inakua nzuri zaidi.
Kuna aina 3 ya resolution maarufu kwa sasa HD Ready(720p), Full HD(1080p) na 4k(2160p au UHD)
1. HD Ready (720p) ina pixels Millioni moja
2. Full HD (1080p) ina pixels Millioni Mbili - Inaonesha vizuri mara mbili zaidi ya HD Ready
3. UHD au Ultra HD (4k) ina pixels Millioni Nne - Inaonesha vizuri mara mbili zaidi ya Full HD
📌 Jitahidi kununua tv ya 4k ili uwekeze kwa baadae. Sasa hivi hata smarphones zinaanza kurekodi video za 4k na muda si mrefu video nyingi zitakuwa na uwezo wa 4k.
Smart TV ni Televisheni yenye uwezo wa kuunganishwa na intanet (mtandao). Smart tv ina uwezo wa ku browse intaneti na kuangalia movies, kusikiliza mziki na taarifa zingine kupitia applikesheni maarufu kama Netflix. Youtube, Spotify n.k
1: Google certified Android Smart TV: hizi TV zimehakikiwa na zinakidhi vigezo vya android na zinakupa uwezo wa kuinstall app yoyote iliyopo Google Play Store.
2: Android Smart TV: hizi smart tv zinatumia pia android operating system lakini haziko certified(hakikiwa). Zinakuwa na aplikesheni chache(aplikesheni maarufu zote zipo) zinazokuja tayari kwenye tv au za ku download.
3: Tizen OS na WebOS: Tizen OS ni operating system ya TV za Samsung na WebOS ni ya tv za LG. Operating system hizi zina aplikesheni maarufu zote.
📌 **Aplikesheni maarufu ni kama Netflix, Amazon Prime, Spotify nk
Mambo mawili ya kuzingatia unapochagua size ya Tv
1: Umbali wa sofa lako na sehemu TV itakapokaa
2: Resolution ya TV
** TV resolution ni namba ya vidoti vidogo sana vinavyotengeneza picha kwenye televisheni yako. Kadri vidoti vikiwa vingi ndivyo picha inakua nzuri zaidi.
Angalia jedwali hili kupata size nzuri tunayopendekeza
📌 Smart tv ni nyembamba sana na muda mwingine zinakua na spika zenye uwezo mdogo wa sauti. Ni vyema ukatumia home theatre, soundbar au subwoofer kuunganisha na TV yako ili ufurahie sauti nzuri yenye ubora na mdundo.
REFRESH RATE
Refresh rate kubwa = Picha nzuri isiyo na ukungu
Contrast ratio kubwa = Picha inaonesha vizuri ikiwa na taarifa zote hata kama scene yake ni ya giza.
📌 OLED TV zina contrast ratio nzuri sana zinazofanya picha iwe na ubora mkubwa.
Matundu(ports) muhimu tv inatakiwa iwe nazo ni HDMI, USB na audio out
1: HDMI
2: USB
3: Bluetooth
4: Audio out
All Rights Reserved @ Impala 2021