Muongozo wa kununua TV na ufahamu wa misamiati yake kama LED, 4K, Smart tv, Android TV na maana zake.
Karibu impala. Leo tutaangalia bei za tv na nini kinafanya TV zingine kuwa na gharama zaidi ya zingine. Bei za TV zinakuwa na utofauti wa bei kutokana na brand, technology, size, kioo na resolution ya TV.
Soma muongozo huu kufahamu kuhusu LED, resolution, size na maneno mengine yanayo tambulisha TV.
Sababu namba moja inayofanya TV ziwe na bei tofauti ni size. Kwa kawaida Size za TV huanzia inch 17 mpaka 100. Bei ya TV inakua kubwa jinsi size inapoongezeka.
Kitu kingine kinachofanya bei ya tv zitofautiane ni aina ya kioo chake. Kuna aina 3 maarufu LED, QLED na OLED. LED huwa na bei ndogo ukilinganisha na QLED na OLED. Utafiti uliofanywa na CNET unaonesha kuwa OLED TV ni bora zaidi ukilinganisha na QLED TV.
Resolution ya TV inachangia pia bei kuwa tofauti. Kwa sasa resolution maarufu ni HD Ready(720p), Full HD(1080p) na Ultra HD(4k). Resolution yenye bei nafuu ni HD ready ikifuatiwa na Full HD na 4k ni gharama zaidi.
Kuna TV za kawaida na Smart TV. Smart tv huwa na gharama sababu ya uwezo wake wa kuunganisha na intaneti ambapo unaweza kuangalia video Youtube na movies Netflix au prime video.
Brand za TV zinahusika moja kwa moja kwenye gharama ya TV. SONY , LG, SAMSUNG zikiwa ni brand ghali sana ukilinganisha na brand kama HISENSE , TCL , EVVOLI, STAR X. Brand zenye bei rahisi ni kama Kodtec, Pinetech, Aborder na Sunrise.
Muunganisho wa sifa zote hizi unafanya TV kuwa na bei tofauti tofauti. Sasa unaweza kununua TV unayo hitaji kupitia impala kwa bei nzuri Tanzania.
All Rights Reserved @ Impala 2021