Tofauti ya Smart TV na Android TV

  • Posted 1 September 2021
  • By Elvis Benjamin

SMART TV - Ni TV inayoweza kuunganishwa na internet. Inakuja na apps maarufu kama Netflix, Youtube, Prime video kwa kuangalia movie na videos. Pia unaweza kutumia browser kutembelea website yoyote kutumia TV yako.

Shida ya smart tv pekee ni kwamba ina apps chache ukilinganisha na Android smart tv. Kwa hivyo apps ulizonazo kwenye simu yako ya android zinaweza zisifanye kazi kwenye hii smart tv ya kawaida.

Soma muongozo huu kufahamu kuhusu LED, resolution, size na maneno mengine yanayo tambulisha TV.

SMART ANDROID TV - Hii ni aina ya smart TV, ina sifa zote za smart tv lakini pia ina apps nyingi kutoka google playstore ukilinganisha na smart tv ya kawaida. Kwenye Smart Android TV, apps ulizonazo kwenye simu yako ya android zinafanya kazi pia kwenye hii TV.

Pia Smart android TV hupokea updates kutoka google mara kwa mara ukilinganisha na smart tv ya kawaida.

Ipi Ununue?

Android TV zinatengenezwa na kampuni chache na huwa na bei kubwa ukilinganisha na smart za kawaida. Mwisho wa siku wewe mwenyewe utachagua ni ipi inafaa. Hapa chini ni baadhi ya android tv tulizonazo impala

Tofauti ya LED na Smart Tv

All Rights Reserved @ Impala 2021