JBL Charge 4, kwa maoni yangu, ndiyo bora zaidi betri, ubora wa sauti, na muundo. Sio kubwa sana na unaweza kubeba kwa urahisi mkononi mwako au kwenye begi bila shida yoyote. Muda wa matumizi ya betri ni masaa 20 na hudumu kwa wiki moja au zaidi kulingana na matumizi yako; pia huchaji haraka sana na inaweza kutumika kama power bank kuchaji vifaa vingine kama simu. Ubora wa sauti ni wa kushangaza. cover la nje limetengenezwa vizuri. ukiweka hii speaker chumba kimoja inasikika nyumba nzima bila jasho. Kwa maoni yangu, inawazidi mbali washindani wake kama vile UE Boom 3, JBL Flip 5, Sony XB32, n.k... Ubora wa muundo na urembo pia ni maridadi. Kama unatafuta portable, premium sounding, spika ya Bluetooth, ningependekeza sana kununua hii. Sababu pekee ingefanya ninunue kitu kama UE Boom 3 au JBL Flip 5 ni urahisi wa kubebeka. Jbl charge 4 ni kubwa kulinganisha na hizo speaker kama flip 5.
Mussa