Size: 128GB
Color: Blue
Hii simu mpya kutoka samsung ni ya kuvutia kwenye sekta zote. Design ya simu hii ni bora sana kimuundo na kimuonekano. Display yake ni kubwa, inch 6.4 Amoled yenye 1080p na refresh rate ya 90Hz inayo fanya simu kuwa smooth unapotumia.
Ina battery Kubwa ya 5000mah inayokaa na chaji muda mrefu (siku 4 na masaa 23). Inachukua dk 45-60 kuchaji kutoka asilimia 0 mpaka 100. SIM card tray ya hii simu ina SIM card 2 na SD card.
Hii simu ina camera 4, main ni 64MP na inapiga picha vizuri wakati wa mchana lakini haina details nyingi wakati wa usiku. Ultra wide camera 8MP nayo kama main camera (haina details wakati wa usiku). Micro camera 5MP nayo ya kawaida na sioni umuhimu wake.
Material ya nyuma na pembeni ya simu hii yapo Kama yametengenezwa na plastic na sio glass. Kwa ujumla hii simu ni nzuri kwa bajeti yake na inafaa sana.